-
Ufafanuzi wa Kina na Maridhawa Juu ya Suala la Unabii Baina ya Waislamu na Wakristo
Sheikh Dk.Alhad Mussa Salum: "Wakristo wanaposema, au tunaposikia ikisemwa, au anapoitwa mtu kuwa ni Nabii au Nabii Mkuu, anaitwa hivyo kwa Istilahi ipi?! Hili ndio swali la msingi kujiuliza?. Anaitwa hivyo kwa Istilahi yetu sisi Waislamu au kwa istilahi yao hao ndugu zetu Wakristo?!. Kwa sababu katika suala la UNABII kila watu wana Istilahi zao".
-
Kauli mbiu: Amani ya Palestina ni Amani ya Tanzania;
Majlis ya Siku ya Kupigwa Upanga Imam Ali (a.s), imefanyika katika Hawza ya Imam Sadiq (a.s), Kigogo, Dar-es-Salam, Tanzania
Maulana Sheikh Hemed Jalala: "Adui Ibn Muljim (laana iwe juu yake), aliyempiga Imam Ali (a.s) kwa upanga wenye sumu kali, alijua kuwa hawezi kupambana na Imam Ali (a.s) akiwa nje ya Msikiti, hivyo akaona mbinu aliyokuwa nayo ni kumuwinda akiwa katika ibada (swala), kwani awapo katika swala huwa mwili wake na hisia zake zinatoweka Duniani, na anazungumza na Mola wake Mtukufu kama vile hayupo Duniani".
-
Hafla ya Ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya Jijini Arusha - Tanzania, kwa jina la Imam Ridha (a.s)
Wasomaji wa Kitaifa na Kimataifa wa Qur'an Tukufu wa Tanzania pamoja na Masheikh waliotoka maeneo mbalimbali ya nchi, ni miongoni mwa waliodhuhuria katika Hafla hiyo adhimu.
-
Habari Pichani | Mkutano wa Washairi na watu wa Utamaduni na Fasihi ya Kiajemi na Kiongozi wa Mapinduzi
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna -, Katika usiku wa kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (amani iwe juu yake), kundi la watu wa Mashairi (Wataalamu wa Fani ya Mashairi) na Utamaduni na Maprofesa wa Fasihi ya Kiajemi wamekuwa wageni wa Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
-
Uzinduzi wa Kituo cha Qur'an - Arusha, Tanzania:
"Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa"
Sheikh Maulid Hussein Kundya amesisitiza juu ya umuhimu wa kuisoma na kuifahamu Qur'an Tukufu, na kuwakumbusha Waumini kuizingatia kauli ya Mwenyezi Mungu ambapo amesema: "Hakika Qur'an hii inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa".
-
Somalia na Sudan zimekataa ombi la kuwapa makazi Wapalestina wanaoishi Gaza
Mamlaka za nchi mbili, Somalia na Sudan, zimekataa katakata pendekezo na mpango wowote kuhusu uhamisho wa Wapalestina wanaoishi Gaza hadi katika eneo la nchi hizi za Kiafrika.
-
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dokta Abubakar Zuber Ali Mbwana:
"Maendeleo sio ugomvi, bali ni kufanya mambo yanayoonekana na yanayompendeza Mwenyezi Mungu"
Msikiti ni Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na ni Kituo cha kiroho, kijamii na kiutamaduni, na vile vile ni nyumba makhsusi kwa ajili ya Waislamu kufanya ibada mbalimbali ndani yake.
-
Nijukumu letu sote kuwapenda na kuwajali Mayatima
"Nijukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anamkumbusha mwenzake juu ya kuwapenda na kuwajali Mayatima na kutatua changamoto zao mbalimbali na kuwatimizia mahitaji yao".
-
"Kutokomeza umaskini miongoni mwa wanawake kutachukua miaka 130"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameashiria matatizo yanayoendelea kuwakabili wanawake na wasichana duniani kote, akionya kwamba "kutokomeza umaskini uliokithiri miongoni mwa wanawake na wasichana kutachukua miaka 130."