11 Agosti 2025 - 10:25
Jeshi la Italia Lawakamata Meli ya Mizigo ya Silaha Inayodaiwa Kutoka Saudi Arabia Kwenda Israel

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, silaha hizo zinadaiwa kuwa sehemu ya mpango mpana wa usafirishaji wa vifaa vya kijeshi kuelekea Israel, wakati huu ambapo mapigano na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza yanaendelea.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Rome, Italia – Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa jeshi la Italia limekamatwa shehena kubwa ya silaha nzito zilizokuwa zikisafirishwa kwa meli ya mizigo kutoka Saudi Arabia kuelekea Israel.

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, silaha hizo zinadaiwa kuwa sehemu ya mpango mpana wa usafirishaji wa vifaa vya kijeshi kuelekea Israel, wakati huu ambapo mapigano na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza yanaendelea.

Ripoti hizo zimezua mijadala mikali katika medani za kisiasa na kijamii, huku wachambuzi wakitafsiri tukio hili kama ishara ya ushirikiano wa karibu kati ya baadhi ya nchi za Kiarabu na serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameeleza wasiwasi wao kwamba misaada ya kijeshi kwa Israel inaweza kuchangia kuendelea kwa mgogoro na ongezeko la vifo vya raia katika Ukanda wa Gaza.

Mamlaka za Saudi Arabia na Israel bado hazijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hili.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha