18 Februari 2026 - 21:43
Katika Ugeni wetu kwa Mwenyezi Mungu, tuvae “Vazi Halisi na Bora Zaidi” la Ucha Mungu!

Katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao ni karamu ya Mwenyezi Mungu, “brand” ya kweli si mavazi ya gharama bali ni taqwa, ikhlasi, subira na maadili mema. Hivi ndivyo vinavyomfanya mja awe mrembo mbele ya Mwenyezi Mungu na kufuzu katika meza ya rehema na maghfira.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Mwaliko maalumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake. Kama ilivyokuja katika hotuba mashuhuri ya Mtume (s.a.w.w):
“Ni mwezi ambao mmealikwa katika karamu ya Mwenyezi Mungu.”

Swali ni hili: Katika karamu hii tukufu, tutavaa vazi gani?!.

Kama tukialikwa kwenye hafla kubwa ya kidunia, tunachagua mavazi yetu bora na ya thamani. Lakini katika karamu ya Mwenyezi Mungu, “Vazi” halisi ni tofauti kabisa:

1- Vazi la Taqwa (Ucha Mungu).

Qur’ani Tukufu inasema:
“Na vazi la Taqwa ndilo bora zaidi.” (Al-A’raf: 26)

2- Vazi la Ikhlasi (Unyofu wa Nia)
Amali inayofanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee, hata ikiwa ndogo, huwa kubwa mbele Yake.

3- Vazi la Subira
Swaumu ni mafunzo ya subira na kujizuia - kujizuia na njaa, kiu na madhambi.

4- Vazi la Ukarimu na Kusaidia Wengine
Ramadhani ni Mwezi wa kuwajali wahitaji na kuilainisha mioyo.

Vazi la Maadili Mema
Mtume (s.a.w.w) amesema: “Swaumu ni ngao.” Ni ngao dhidi ya hasira, uongo na dhulma.

Katika Karamu hii, si sura ya mavazi inayoangaliwa wala majina ya chapa za dunia; kinachoangaliwa ni usafi wa moyo, nia safi na matendo mema.

Basi na tuvae katika Karamu ya Mwenyezi Mungu vazi la Taqwa, tujipake manukato ya dhikri, na tujipambe kwa maadili mema - kwani “Mavazi” haya hayapotezi thamani zake, na malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu peke Yake.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha