13 Julai 2026 - 23:54
Kiongozi wa Mapinduzi: Kulipiza kisasi hakutategemea uwepo wangu au wa viongozi wengine

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kuwawajibisha waliohusika na mauaji ya Kiongozi Shahidi ni jambo ambalo litaendelea bila kutegemea uwepo wake binafsi au wa viongozi wengine, akisisitiza kuwa watu huru duniani watatekeleza wajibu wao kwa wakati wake.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa suala la kuwawajibisha waliohusika na mauaji ya Kiongozi Shahidi wa Iran halitegemei uwepo wake binafsi wala wa viongozi wengine.

Katika sehemu ya ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Iran, alisema kuwa wahusika wa mauaji hayo hawapaswi kudhani kuwa mchakato wa kulipiza kisasi au kuwajibishwa utasitishwa kutokana na kutokuwepo kwa viongozi fulani.

Tuwepo au tusiwepo, jambo hili litatimia. Hivi karibuni, watu huru katika maeneo mbalimbali duniani, kila mmoja atatekeleza sehemu ya jukumu hili la Mwenyezi Mungu.”

Kiongozi wa Mapinduzi alisisitiza kuwa dhamira ya kusimamia haki na kuwawajibisha wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo itaendelea, akieleza kuwa watu huru katika sehemu mbalimbali za dunia wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa imani na misingi wanayoifuata.

Kauli hiyo imejumuishwa katika ujumbe alioutoa kwa mnasaba wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Iran, uliolenga kuwapa pole wananchi wa Iran, kuenzi mashahidi wa vita vya hivi karibuni na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kushikamana katika kulinda misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha