Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limefanya mashambulizi ya makombora ya balestiki dhidi ya vituo vya kimkakati na maeneo ya wanajeshi wa Marekani katika kambi moja ya anga nchini Jordan, ikiwa ni sehemu ya awamu ya tatu ya wimbi la pili la Operesheni "Nasr-2".
Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya IRGC na kunukuliwa na Shirika la Habari la IRNA, jeshi hilo limesema kuwa operesheni hiyo ilitekelezwa alfajiri ya Jumanne kwa kaulimbiu "Ya Litharat al-Husayn (as)" / "Ewe mlipiza kisasi cha Imam Husayn (as)!" ikisema kuwa kambi hiyo ilitumiwa na jeshi la Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makombora ya balestiki yalilenga miundombinu ya kimkakati na maeneo ya wanajeshi wa Marekani katika kambi hiyo, huku IRGC ikisema kuwa shambulio hilo lilikuwa ni jibu kwa hatua za kijeshi za Marekani.
Aidha, IRGC imedai kuwa katika siku ya kwanza ya mashambulizi dhidi ya Iran, Marekani ilitumia kambi hizo kushambulia mji wa Minab kusini mwa Iran, na kusababisha vifo vya wanafunzi 168 pamoja na walimu wao.
Madai haya yametolewa na IRGC na hayajathibitishwa kwa kujitegemea wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii.
Your Comment