-
"Jina langu ni Mahmoud Khalil, mimi ni mfungwa wa kisiasa"
Mahmoud Khalil, mwanafunzi wa Kipalestina katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani, amejieleza kama mfungwa wa kisiasa katika maoni yake ya kwanza tangu alipokamatwa na vyombo vya usalama vya Marekani kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya watetezi wa Palestina.
-
'Waislamu wachukue msimamo wa maana dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni'
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq ya An-Nujabaa imelaani mashambulizi ya kinyama yaliyoanzishwa tena na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kuwataka Waarabu na Waislamu duniani kote wachukue misimamo thabiti dhidi ya hujuma hizo.
-
Maafisa 5 waandamizi wa HAMAS wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel Ghaza
Maafisa watano waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Hamas: Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika vita dhidi ya watu wa Gaza
Msemaji wa harakati ya Hamas amesema harakati hiyo inatekeleza kikamilifu masharti ya makubaliano ya usitishaji vita na kwamba Wazayuni wameyakiuka akisisitiza kuwa, uratibu wa awali wa utawala huo ghasibu na Washington wa kuanzisha tena vita dhidi ya watu wa Gaza unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika jinai zinazofanywa Wazayuni.
-
Al Houthi: Israel inapanga kushambulia nchi zingine ikiwa itaangamiza Palestina
Kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuwa utawala ghasibu wa Israel utaanza kushambulia nchi nyingine ikiwa utafanikiwa kuangamiza juhudi za ukombozi za Palestina dhidi ya ukaliaji na uchokozi wake, huku akipendekeza hatua za kijeshi na nchi za Kiarabu na Kiislamu dhidi ya utawala huo.
-
Dunia yakasirishwa na hatua ya Israel kuendeleza vita dhidi ya Gaza
Jamii ya kimataifa imebainisha hasira yake baada ya utawala katili wa Israel kuendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza, huku ikivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa na lengo la kumaliza mzozo wake wa miezi 17 na Hamas.
-
Iran yakosoa vikali uingiliaji wa nchi za Magharibi katika kazi za Baraza la Haki za Kibinadamu UN
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amezikosoa vikali baadhi ya nchi za Magharibi kwa kutumia vibaya taasisi za Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa, nchi hizo zinataka kuingiza siasa katika masuala ya haki za binadamu dhidi ya Iran kwa kupuuza masuala ya kimsingi ya haki za binadamu ukiwemo mgogoro wa Palestina.
-
Masharti ya Iran katika kufanya mazungumzo na nchi za Magharibi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza wazi masharti yake ya kufanya mazungumzo na nchi za Magharibi, huku ikisisitiza kutofanya mazungumzo yaliyosimama kwenye msingi wa mashinikizo na vitisho.
-
Katibu Mkuu wa UN asema ameshtushwa na mashambulio mapya ya Israel Ghaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, ameshtushwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza yaliyoua shahidi mamia ya Wapalestina wakiwemo watoto na wanawake.
-
Iran imeuza madini yenye thamani ya dola bilioni 12 katika kipindi cha mwaka mmoja
Mauzo ya nje ya madini ya Iran yameongezeka katika miezi 11 ya mwaka wa Kiirani hadi mwishoni mwa Februari, yakifikia jumla ya dola bilioni 12.599.
-
Human Rights Watch: Afghanistan si salama kwa wahamiaji waliofukuzwa kutoka Pakistan
Human Rights Watch, katika ripoti yake ya hivi punde kuhusu wahamiaji wa Afghanistan nchini Pakistan, ilionyesha wasiwasi wake kuhusu kufukuzwa kwa lazima kwa wahamiaji hao.
-
Tangazo la Urusi la kuwa tayari kupatanisha Pakistan na Afghanistan
Wakati mvutano kati ya Pakistan na Afghanistan ukiendelea, Balozi wa Urusi nchini Pakistan alitangaza utayari wa nchi yake kutatua mivutano hii.
-
Ripoti ya Picha | Usomaji wa Qur'an Tukufu huko Kandahar, Afghanistan
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S.) - Abna - Programu ya kisomo cha Qur'an Tukufu hufanyika kila siku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Sadeghieh wa Kandahar, Afghanistan.
-
Wakimbizi wapya 13,000 wa Syria wamekimbilia Lebanon / wakikimbia uhalifu wa Al-Julani kwenye Pwani ya Syria
Takriban wakimbizi wapya elfu 13 wa Syria wameingia katika vijiji na miji 23 Kaskazini mwa Lebanon.
-
Ripoti ya Picha | Ushiriki wa Mashia wa Tanzania katika programu maalum za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Vipindi maalum vya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani vinafanyika katika vituo 11 vya Kidini nchini Tanzania kwa kushirikisha Mashia wa nchi hii chini ya Uongozi na Mpango wa Taasisi ya Hojjatul- Asr (a.t.f.s) ya Tanzania.
-
Marasimu ya kuhuisha Mikesha ya Siku za Lailatul-Qadr itafanyika katika Haram ya Hadhrat Zainab (s.a)
Marasimu (Sherehe) ya kuhuisha Usiku wa Lailatul- Qadr itafanyika kwa muda wa nyusiku tatu katika Madhabahu (Haram) Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a).
-
Ripoti ya Picha | Hafla yaUzinduzi wa Tafsiri ya Qur'an Tukufu kwa Lugha ya Kiswahili nchini Tanzania
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - ABNA - Hafla ya uzinduzi wa Tafsiri ya Qur'an Tukufu kwa Lugha ya Kiswahili iliyoandikwa na Marehemu Sheikh Hassan Ali Mwalupa (Mwenyezi Mungu Amrehemu) imefanyika nchini Tanzania. Wafuasi wa Madhehebu mbalimbali za Kiislamu nchini Tanzania, wakiwemo Mashia wa Khoja wa nchi hii ni miongoni mwa waliohudhuria katika hafla hii.
-
Takriban Maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa Shahidi katika Mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza
Takriban maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.
-
Fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan:
Tusiwe wavivu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na tusichoke kuomba Maghfira na Msamaha
Kila kizuri unachokifanya ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ni thawabu.Hata pumzi zetu tunapopumua ndani ya Mwezi huu, hilo linahesabiwa kuwa ni ibada, na hata kulala kwetu na usingizi wetu ndani yake pia ni ibada. Sisi ni wageni wa Mwenyezi Mungu ndani yake.
-
Vi[indi vya Tafsiri ya Qur’an Tukufu:
Tafsiri ya Aya ya Kwanza ya Surat Al-Maidah
Kwa kuwa "Hakika ya Waumini ni ndugu", basi Muislamu anatakiwa kuhakikisha kuwa anatimiza Haki ya ndugu yake Muislamu, na anatetea Haki yake kama Muislamu na kama ndugu yake.
-
Imetolewa Katika Mkutano wa Ukosoaji wa Mfululizo wa Muawiyah:
Mfululizo wa filamu ya “Muawiyah”, Ni utekelezaji wa amri za Kiwahabi / Ili kuvutia hadhira badala ya kusimulia Historia halisi!
Katika mkutano wa mapitio ya mfululizo wa filamu ya “Muawiyah”, wataalamu walizingatia lengo kuu la mfululizo huu kuwa ni utakaso wa Bani Umaiyya na Muawiyah, na ni upotoshaji wa Historia kwa kupendelea Uwahabi, na ni katika kukamilisha mradi wa migogoro baina ya Shia-Sunni.
-
Video | Usomaji wa Tawashih ya (Asma -ul- Husna) kwenye Staha ya Meli ya Kivita ya Iran
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna - Kikundi cha Tawashih kiitwacho: Muhammad Rasulullah (s.a.w.w) kimefanya tukio la Usomaji wa Tawashih ya "Asma -ul- Husna" kwenye sitaha ya Meli za kivita za Dana na Rudaki za Iran.
-
Ayatollah Nouri Hamedani: Utawala wa Kizayuni unaoua watoto kwa mara nyingine tena umeonyesha kwamba hauzingatii ahadi zozote
Ayatollah Nouri Hamedani ametoa ujumbe akilaani jinai za hivi karibuni za Marekani na utawala wa Kizayuni na kusema: Leo hii utawala wa Kizayuni unaoua watoto kwa mara nyingine umeonyesha tena kwamba haufuatilii (na hauzingatii) ahadi zozote na unavunja ahadi (mapatano) kirahisi.
-
Vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza vimeanza tena| Wapalestina 131 wameuawa Shahidi katika mashambulizi ya mabomu ya ndege za Israel
Utawala wa Kizayuni umeshambulia kwa mabomu maeneo mbalimbali ya makazi ya watu katika Ukanda wa Ghaza
-
Ushahidi wa Mawalii Katika Kumfananisha Ali na Manabii
Ali (a.s), wapo Watu waliodai kuwa wanampenda, mpaka wakamfanya kuwa ni mungu, ametakasika Mwenyezi Mungu na wanayo mshirikisha nayo. Na wapo watu waliomchukia na wakampiga vita, wakamtukana na kumlaani, wakakufuru na wakatoka katika Uislamu. Na wapo baadhi ya Watu waliompenda, wakawa watiifu kwake, na wakashikamana naye kama alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w), basi kwa hakika hao ndio waumini wa kweli.
-
Hafla ya Ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya Jijini Arusha - Tanzania, kwa jina la Imam Ridha (a.s)
Wasomaji wa Kitaifa na Kimataifa wa Qur'an Tukufu wa Tanzania pamoja na Masheikh waliotoka maeneo mbalimbali ya nchi, ni miongoni mwa waliodhuhuria katika Hafla hiyo adhimu.
-
Ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya - Jijini Arusha, Tanzania
Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Leo hii (jana 17/3/2025) kumefanyika tukio muhimu kwa wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s) Jijini Arusha, nalo ni ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya kwa jina la Imamu Ridha (a.s), chini ya Usimamizi wa Taasisi ya Sayyid al-Shuhadaa (a.s), inayoongozwa na Samahat Sheikh Maulid Hussein Kundya.
-
Swali kuhusu kadhia ya Palestina:
Ni kwa nini Mashia tu ndio wako mstari wa mbele kwenye kulitetea suala la Palestina?!
Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge: "Uislamu usiokuwa wa Ahlulbayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), huo umetengenezwa na Mayahudi au kama haukutengenezwa na Mayahudi basi umeingizwa mikono kwa asilimia 99% na Mayahudi".
-
Ayatollah Nouri Hamedani: Jumuiya za Kisayansi za Hawza, ni mahala salama kwa mawazo mapya na safi
Ayatollah Nouri Hamedani Marjii Taqlid wa Madhehebu ya Shia ametoa ujumbe wake katika Mkutano wa vyama (jumuiya) vya Kisayansi vya Seminari (Hawza) ya Qom.
-
Kwa nini Israel na Marekani zinaeneza chuki dhidi ya Uislamu kwa kutumia vibaya vyombo vya habari?
Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zimeendeleza vitendo vyao vya uharibifu na kuiondoa Televisheni ya Al-Aqsa katika satalaiti zote za kimataifa kwa lengo la kubana uhuru wa kujieleza.