11 Septemba 2025 - 09:38
Israel imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya Sanaa (Mji Mkuu wa Yemen) na Mkoa wa Al-Jawf

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Yemen, mashambulizi ya Israeli yaliyoelekezwa Sanaa na Mkoa wa Al-Jawf yamesababisha watu wasiopungua 35 kuuawa na zaidi ya 130 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Jeshi la anga la utawala wa Kizayuni (Israel) limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya mji mkuu wa Yemen, Sana'a, na kulenga majengo ya serikali ya Ansarullah.

Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni:

  • Jengo la Wizara ya Ulinzi la serikali ya Ansarullah katikati ya mji mkuu,

  • Ofisi ya Rais,

  • Kituo cha Amri na Udhibiti wa Jeshi,

  • Maeneo ya kijeshi katika Jabal al-Hafa,

  • Kituo cha umeme cha Haziz,

  • Kituo cha usambazaji wa mafuta kilichokuwa kikihudumia magari ya wagonjwa na misaada ya dharura,

  • Nyumba za viongozi wa Ansarullah,

  • Na pia shirika la habari la Saba, linaloendeshwa na serikali ya Ansarullah.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ya Yemen, mashambulizi haya yamesababisha vifo vya idadi kadhaa ya watu na kujeruhiwa kwa wengine katika mikoa ya Sana’a na Al-Jawf.

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa mashambulizi haya yalikuwa na malengo mahsusi na yalitekelezwa kwa amri ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha