Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, akiwa ameongozana na wajumbe wa ngazi ya juu wa kidiplomasia, ameondoka kuelekea katika eneo la kufanyika mazungumzo na Marekani mjini Muscat, Oman, asubuhi ya siku ya Ijumaa.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kujikita katika masuala muhimu ya pande mbili na ya kikanda, yakiwemo faili la nyuklia, vikwazo vya kiuchumi, pamoja na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati, huku kila upande ukitarajiwa kuwasilisha misimamo na mapendekezo yake katika juhudi za kutafuta mwafaka wa kidiplomasia.
Your Comment