Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Jeshi la anga la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (Islamic Revolutionary Guard Corps) limetangaza kuwa limefanya shambulizi la makombora dhidi ya maeneo manne ya kijeshi ya Marekani nchini Jordan.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imesema kuwa wapiganaji wa kikosi cha anga cha walinzi hao walilenga na kuharibu maeneo muhimu kwa kutumia makombora ya masafa marefu yanayotumia mafuta gumu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shabaha zilizoathiriwa ni pamoja na hangari za ndege za kivita aina ya F-35 pamoja na kituo cha amri na udhibiti kilichopo katika kambi ya kijeshi ya Al-Azraq, ambayo imetajwa kuwa inatumiwa na jeshi la Marekani.
IRGC imesisitiza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya majibu yake dhidi ya kile ilichokiita vitendo vya uchokozi vinavyolenga Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikisisitiza kuwa itaendelea kujibu kwa nguvu dhidi ya vitisho vyovyote vinavyotoka nje.
10 Juni 2026 - 12:57
News ID: 1825342
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) wamedai kufanya mashambulizi ya makombora yaliyolenga maeneo manne muhimu ya kijeshi ya Marekani katika kambi ya Al-Azraq nchini Jordan, ikiwa ni pamoja na kituo cha amri na udhibiti.
Your Comment