-
Mamia ya Waislamu wahofiwa kufariki katika tetemeko la ardhi Myanmar
Mamia ya Waislamu wanahofiwa kuwa miongoni mwa watu zaidi ya 1,600 waliopoteza maisha katika tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katikati ya Myanmar, wakati walipokuwa wakiswali misikitini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Waziri Mkuu wa Greenland amjibu Trump: Marekani haitakipata kisiwa hiki
Waziri Mkuu wa Greenland amejibu matamshi ya Rais wa Marekani aliyedai kwamba Washington inataka kukidhibiti kisiwa hicho kikubwa cha ncha ya kaskazini ya dunia, na kusisitiza kwamba: "Marekani haitaipata Greenland".
-
Ripoti: Wamarekani wanahamia Mexico kukwepa sera za kibaguzi za Trump
Katika jitihada za kukwepa siasa na sera za Rais Donald Trump wa chama cha Republican, Wamarekani, baadhi yao wakiwa na asili ya Mexico, wanahamia nchi jirani ya Mexico, katika kile kinachoweza kutambuliwa kuwa uhamiaji wa kinyume.
-
Marekani, Mshirika Asiyeaminika
Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, ambaye amemrithi Justin Trudeau, amesisitiza kwamba atajibu hatua za Marekani dhidi ya nchi hiyo katika nyanja za kiuchumi na kibiashara, na amekiri kwamba: "Marekani si mshirika wa kuaminika tena."
-
Wanachuo 300 wapokonywa viza US kwa kuiunga mkono Palestina
Marekani imebatilisha viza za wanafunzi zaidi ya 300 wa kigeni kwa kuratibu na kushiriki katika maandamano ya kuwanga mkono na kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina katika mabewa ya vyuo vikuu kote nchini humo.
-
Takriban watu 20 Wameuawa baada Wanajeshi wa Nigeria kushambulia Maandamano ya Siku ya Quds Mjini Abuja
Makumi ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina wameuawa na kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuwafyatulia risasi wakiwa kwenye Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika Mji Mkuu wa Nigeria.
-
Marekani na Ulaya zashindwa kukabiliana na changamoto za kimataifa
Mark Rutte, Katibu Mkuu wa NATO amesisitiza juu ya umoja wa pande mbili za Bahari ya Atlantiki na kusema kuwa changamoto za kiusalama duniani ni kubwa kiasi kwamba Ulaya na Marekani pake yazo haziwezi kukabiliana nazo.
-
Kutozwa ushuru wa asilimia 25 na Marekani kwa nchi zinazonunua mafuta ya Venezuela
Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa biashara yoyote na nchi zinazonunua mafuta na gesi ya Venezuela. Ameelezea ushuru huu kama jibu la kutumwa Marekani wanachama wa genge la uhalifu la "Tren de Aragua".
-
Trump asaini amri ya kubadilisha mfumo wa uchaguzi na upigaji kura Marekani, apingwa vikali
Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya kiutekelezaji ya kubadilisha mfumo wa uchaguzi na upigaji kura wa nchi hiyo, inayojumuisha sharti la uthibitisho wa uraia kwa usajili wa wapiga kura.
-
Google kutumia majasusi wa Israel waliohusika na mauaji ya kimbari ya Gaza
Kampuni ya Google mapema wiki hii ililipa dola bilioni 32 ili kununua kampuni ya Israel ya usalama wa mtandao, Wiz, ambayo inaendeshwa na wafanyakazi wa zamani wa Unit 8200, kitengo maalumu cha upelelezi wa mtandao cha jeshi la Israel.
-
Waziri Mkuu wa Canada: Hatimaye Trump ataonyesha heshima kwetu na atataka mazungumzo
Waziri Mkuu wa Kanada Mark Carney amesema mazungumzo mapana ya kibiashara baina ya nchi yake na Marekani hayatafanyika mpaka pale Trump atakapoonyesha heshima kwa uhuru na mamlaka ya kujitawala ya Canada.
-
China yaionya Marekani, yaitaka iache kuingilia ushirikiano wake wa kibiashara na Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameionya Marekani kwa kuitaka iache kuingilia ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya China na Iran.
-
Trump atahadharishwa: Vita na Iran havifanani na utembeaji kwenye 'maonyesho ya mitindo'
Ted Galen Carpenter, mchambuzi mashuhuri wa masuala ya kijeshi wa Marekani amemtahadharisha rais wa nchi hiyo Donald Trump na matokeo hatari ya kuanzisha vita dhidi ya Iran.
-
Moto mpya wa vita wawashwa na utawala wa Kizayuni huko Gaza kwa msaada wa Marekani
Kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza yaliyoanza kutekelezwa tarehe 19 Januari, utawala wa Kizayuni umeanzisha tena vita vya umwagaji damu dhidi ya eneo hilo lililoharibiwa na vita, kwa kufanya mashambulizi makubwa ya kinyama ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya mashahidi wa Kipalestina na kujeruhi wengine wengi katika ukanda huo.
-
Onyo la Iran kwa Marekani kuhusu matokeo mabaya ya uchokozi wa aina yoyote
Amir Saeed Irvani, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa alitahadharisha katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kwamba, hatua zozote za kichokozi zitakazofanywa na Marekani zitakuwa na matokeo mabaya na hatari mno.
-
Adhanom: Kukatwa misaada ya Marekani kunatishia maisha ya mamilioni ya watu
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonya kwamba kukatwa ufadhili wa Marekani kwa shirika hilo, mipango yake ya afya na mashirika mengine kunatishia uhai wa mamilioni ya watu.
-
"Jina langu ni Mahmoud Khalil, mimi ni mfungwa wa kisiasa"
Mahmoud Khalil, mwanafunzi wa Kipalestina katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani, amejieleza kama mfungwa wa kisiasa katika maoni yake ya kwanza tangu alipokamatwa na vyombo vya usalama vya Marekani kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya watetezi wa Palestina.
-
Katibu Mkuu wa UN asema ameshtushwa na mashambulio mapya ya Israel Ghaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, ameshtushwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza yaliyoua shahidi mamia ya Wapalestina wakiwemo watoto na wanawake.
-
Kwa nini Israel na Marekani zinaeneza chuki dhidi ya Uislamu kwa kutumia vibaya vyombo vya habari?
Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zimeendeleza vitendo vyao vya uharibifu na kuiondoa Televisheni ya Al-Aqsa katika satalaiti zote za kimataifa kwa lengo la kubana uhuru wa kujieleza.
-
Canada kuangalia upya mkataba wa kununua ndege za kivita za Marekani
Waziri Mkuu mpya wa Canada, Mark Carney ametoa amri ya kupitiwa upya mkataba wa nchi hiyo na kampuni ya silaha ya Marekani unaohusiana na kuiuzia Canada ndege za kivita za F-35.
-
Hatua ya Marekani ya kuishambulia kijeshi Yemen; kukariri mkakati ulioshindwa kufua dafu mbele ya Ansarullah
Donald Trump, ambaye aliingia madarakani kwa ahadi ya kuleta suluhu na amani na kuhitimisha vita kadhaa wa kadhaa vilivyoanzishwa na Marekani, ametoa amri ya kushambuliwa kijeshi Yemen baada ya kupita miezi miwili tu tangu ashike hatamu za utawala.
-
UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake juu ya "ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu", akitoa wito kwa serikali kulinda uhuru wa kidini, na kwa majukwaa ya mtandaoni kuzuia matamshi ya chuki.
-
Utawala wa Trump kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43
Gazeti la New York Times limeandika katika toleo lake la leo kuwa serikali ya Donald Trump inapitia mpango wa kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43.
-
Utawala wa Trump wazidisha ukandamizaji dhidi ya wanafunzi wanaoitetea Palestina
Hatua ya serikali ya Marekani ya kumtia mbaroni mwanaharakati anayepinga vita na anayeunga mkono Palestina anayepata elimu nchini humo imezidisha wasiwasi kuhusu kushadidi makabiliano ya kiusalama na watetezi wa Wapalestina na vuguvugu la wanafunzi nchini Marekani.
-
Muirani afutwa kazi Marekani kwa kuwa AI imesema anaunga mkono Palestina
Chuo Kikuu cha Yale cha nchini Marekani kimemsimamisha kazi mhadhiri wa Kiirani kwa tuhuma zilizotegemea ripoti ya Akili Mnemba (Artificial Inteligence) ambayo imesema kuwa msomi huyo Muirani analiunga mkono taifa madhlumu la Palesitna hasa kutokana na kukosoa vikali mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israeli wakati wa vita vya Ghaza.
-
Maandamano dhidi ya Trump na Musk kila siku Washington DC
Mji mkuu wa Marekani, Washington DC, unaendelea kushuhudia maandamano ya karibu kila siku dhidi ya Rais Donald Trump kutokana na hatua zake za kuwaachisha kazi wafanyakazi, kubana matumizi na kusaini maagizo ya kiutendaji ambayo yanakiuka maslahi ya nchi.
-
Jamaatul-Islami yaitahadharisha serikali ya Pakistan isihadaiwe na hila za Trump
Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Jamaat-e-Islami Pakistan (JIP) ameihutubu serikali ya Islamabad akisema: Marekani si yenye kuitakia kheri katu Pakistan na haipasi kuridhia matakwa ya nchi hiyo.
-
Wacanada wenye hasira wamjibu kivitendo Donald Trump
sambamba na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuongeza mashinikizo kwa Ottawa nwa vitisho vyake vya kuiteka Canada na kuijumuisha kwenye majimbo ya Marekani, wananchi wenye hasira wa Canada nao wameamua kutokaa kimya na wameanza kwa nguvu kutekeleza vikwazo dhidi ya bidhaa za Marekani.
-
UN: Utawala wa Trump uache kuingilia uhuru wa mahakama
Ripoti Maalumu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua za hivi majuzi za serikali ya Donald Trump ya kuwatimua na kuwateua maafisa wapya wa mahakama, akielezea wasiwasi wake kwamba hatua hizi ni sehemu ya vitisho kwa uhuru wa mfumo wa mahakama wa Marekani.
-
Wainjilisti wamshinikiza Trump kulipa wema, wamtaka aruhusu kunyakuliwa Ukingo wa Magharibi
Ripoti iliyochapishwa katika gazeti la Marekani, The New York Times, imefichua kwamba Wakristo wa Kiinjilisti, ambao walitoa huduma kubwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati wa uchaguzi uliopita, ambapo karibu asilimia 80 walimpigia kura, sasa wanasubiri alipe fadhila na kuiruhusu Israel kutwaa Ukingo wa Magharibi, kwa madai ya ahadi ambayo eti Mungu aliwaahidi Wayahudi katika Biblia.